KARIBU JIKONI

Tollyzkitchen Boresha Mapishi Nyumbani

 

Tolly Ben

Tolly Ben

   UTANGULIZI

Tollyzkitchen ni jiko linalofundisha juu ya chakula na mapishi.Jiko hili huendeshwa na Mtanzania  katika Lugha ya kiswahili kwa ajili ya watumiaji wote wa lugha  ya kiswahili. ……………………………………………………………………..

 

 

MALENGO

Moja:Kuboresha mapishi nyumbani

Ingawa Afrika ni Bara lililobarikiwa na vyakula vingi, Ufahamu na ujuzi wa kuandaa chakula Bora chenye ladha nzuri,muonekano wakuvutia na wingi wa virutubisho ni mdogo kwa waafrika wengi.Jiko hili liko hapa kutatua tatizo hili

Mbili:Kuielimisha jamii juu ya virutubisho vya chakula na umuhimu wake katika mwili.

Elimu ndogo juu virutubisho vya chakula na umuhimu wake katika mwili huwafanya watu wengi wale mlo usio kamili,hivyo kusababisha ukosefu wa virutubisho muhim mwilini na kua chanzo cha magonjwa mbalimbali katika jamii.jiko hili hutoa elimu juu ya virutubisho vya chakula na umuhim wake katika mwili.

Tatu:Kukuza matumizi ya bidhaa za chakula zinazozalishwa Nchini 

Nchi nyingi za Afrika huzalisha bidhaa za chakula. Ingawa bidhaa hizo ni nyingi sana sokoni,watu wengi hupenda kununua na kutumia bidhaa za chakula zitokazo nje.Jiko hili huamasisha waafrika kutumia bidhaa za chakula zinazozalishwa katika nchi zao, kwani bidhaa hizo ni bora na fresh kuliko zile zitokazo nje.Hili litachangia maendeleo na ukuaji wa viwanda vya usindikaji wa  vyakula na kukuza uchumi wa nchi za Afrika

DIRA

Dira ya Tollyzkitchen ni kua jiko linalotoa elimu na mafunzo bora ya upishi,chakula na virutubisho,na kuboresha upishi na ulaji wa virutubisho sahihi vya chakula kwa watanzania na watu watumiao lugha ya Kiswahili.Kuona watanzania wakitumia bidhaa za chakula zinazozalishwa hapa nchini.

DHIMA

 • Kutoa Elimu na mafunzo ya upishi,chakula na lishe bora kwa kupitia,tovuti ,simu,redio ,runinga ,vitabu na mafunzo kwa vitendo.
 • Kutoa ushauri na maelekezo juu ya chakula na lishe kwa makundi maalum
 • Kutoa Elimu juu ya chakula na virutubisho kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ,kwa kushirikiana na taasisi za elimu
 • Kufundisha na kuelimisha jamii juu ya upishi,vyakula na lishe bora kwa kutumia michezo,mashindano,muziki na sanaa mbalimbali.
 • Kukuza na kuboresha matumizi ya bidhaa za chakula zinazozalishwa hapa nchini kwa kutoa elimu ya uelewa na utambuzi wa bidhaa bora za chakula.

KWA MAPISHI NA RECIPES BOFYA  CATEGORIES UIPENDAYO KULIA KWAKO

300 Comments

300 thoughts on “

 1. Hodii humu ndani. Nafurahi kuwa kwenye jiko hili manake kwa muda sasa nimekuwa nikipata recipes humu ndani, sasa nimeamua kujiunga kabisa ili nisipitwe! Big up Tollyzkitchen!!

 2. Napenda sana kutembelea jikoni kwako nilifuata maelekezo ya jinsi ya kupika pancakes nikapika vizuri sana I love it

 3. nahtaji kuwa mwanafamilia wa jikoni ili kuboresha afya bora niwapo mjamzito, mtoto na ndoa yng.

 4. napenda sana maswala ya upishi kwa kweli lazima nifuate jiko lako kiukweli lina mafundisho mazur

 5. hodiiiiiiiii……nimeipenda sana hii kitu my.be blssng sana napend sn kupka kwa kweli maan mume wangu anapenda kula home sn hasa asubh na jioni. thx mamy.

 6. Nimependa hii site, ninakuja na ombi kwako. Naomba unisaidie a full diet weekly schedule. Mfano asubuhi: (vyakula vinavyo faa kuwepo kwenye menu), mchana na jioni pia. Natamani sana kuwa nakula balanced diet kila siku ila sifahamu vizuri huu mpangilio. Kama inawezekana ntashukuru @tollyzkitche

 7. Nimependa page yenu utufundishe vyakula vinavyosaidia kuondoa kitambi since tatizo hilo limekuwa kubwa

 8. Lol finally nimejiunga na jiko hili maana nilikuwa natolea macho tu kupitia instagram yako.. kazi nzuri mpendwa na Mungu akuzidishie

 9. Asanteni Sana Kwa Kunifanya Niwe Mtu Ninayependwa Kutembelewa Na Wageni. Hasa Ktk Kupata Chakula Kiwavutiacho. Pia Wao Kujifunza Tokea Kwangu. GOD BE WITH U.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s