Archives

MAJI YA TANGAWIZI NA MDALASINI


Siku hizi zakaribuni mvua imekua ikinyesha kwa wingi na hali yahewa ni baridi kwa baadhi ya mikoa hapa nchini.Watu hukabiliana na baridi hiyo kwa njia na namna mbalimbali.Hapa jikoni tunakabiliana na baridi kwa kikombe  cha Maji vuguvugu yenye Tangawizi,mdalasini na asali.

015

Tangawizi na mdalasini vinasifa yakuleta joto mwilini kwa haraka na pia huongeza uwezo wa mwili kumeng’enya na kutumia chakula  (Metabolism).Sifa hizi hufanya viungo hivi kua moja ya viungo muhimu katika kuiweka afya yako salama.Unaweza tumia viungo hivi hata katika mapishi mengine

Mahitaji

 • Maji yamoto kikombe 1
 • Tangawizi kijiko 1 cha chai (inaweza kua yaunga,au sugua tangawizi mbichi kisha kamua maji yake)
 • Mdalasini ½ kijiko chai ( wa unga/uliosagwa)
 • Asali Mbichi  kijiko 1 cha chai

Njia

1.Chemsha maji adi yatokote

2.Katika kikombe weka Tangawizi na mdalasini,kisha mimina maji yamoto.Koroga ili kuchanganya.Funika kikombe kwa dakika tano

 •  Funika kikombe ili kutunza virutubisho na kutunza joto ili liwezeshe uvunaji wa virutubisho kwenye viungo
 • Usichemshe viungo jikoni kwani kufanya hivyo kutapoteza virutubisho na nguvu ya viungo

3.Ongeza asali,koroga .Tayari kwa kunywa.

 • Asali huongezwa baada ya joto la maji kupungua ili kuepuka kuuwa enzymes walio kwenye asali,pamoja na kutunza virutubisho vilivyo kwenye asali
 •  Chuja kabla yakunywa ukipenda

Tafiti za Tiba lishe na virutubisho zinaonyesha kwamba ni lazima kutumia tangawizi kijiko kimoja cha chai Wakati wowote unapotumia tangawizi kama tiba lishe ili kupata matokeo

Naamini kinywaji hiki kitakufaa sana siku za baridi

JUISI YA MAEMBE NA UBUYU??!!! HERI YA MWAKA MPYA 2014


HERI YA MWAKA MPYA .Ni mwaka mwingine MUNGU ametupa na tunakila sababu yakumshukuru.Naamini tumeuona mwaka huu kwasababu MUNGU bado anamakusudi na maisha yetu.

Juisi ya Maembe na ubuyu

Juisi ya Maembe na ubuyu

Asante sana kwakua nasi 2013,uwepo wako hapa jikoni umetufikisha hapa tulipo.Kama si kwawapenzi wajiko hili kama wewe basi nina hakika jiko hili lisingekua hivi lilivyo leo. Asante sana kwa sapoti yako na naamini tutakua wote 2014

Ni imani yetu kwamba 2014 utakua mwaka mzuri sana hapa jikoni, Tumejipanga kukupa mambo mazuri na kuboresha upishi wako.

Naamini wengi wetu hufrahia  sana msimu wa maembe unapofika na nihuzuni kwetu msimu huo unapokwisha.Ingawa nijambo la kawaida sana kutengeneza juisi ya matunda mchanganyiko, ni mara chache sana au si kawaida kwa wengi kuchanganya ubuyu na matunda mengine.

Wengi hawahesabu ubuyu katika kundi la matunda  hivyo huwawia vigumu kuwaza kuchanganya ubuyu na matunda mengineili kupata juisi nzuri

Mahitaji

 • Ubuyu (wa unga au mbegu) chemsha na maji  kiasi uku ukikoroga,acha ipoe kisha chuja,weka pembeni
 • Maembe .osha,menya ,kata kisha saga na maji kiasi,chuja,weka pembeni
 • Sukari
 • Maji
 • Tangawizi (kwa anaependa si lazima)

Njia

1.Saga tangawizi iwe laini sana,katika sufuria changanya tangawizi  na maji kiasi,funika sufuria kisha chemsha adi maji yatokote.chuja,acha ipoe.

2..katika chombo kikubwa changanya juisi ya ubuyu na juisi ya maembe na maji ya tangawizi  ,ongeza maji ili kupata uzito uupendao kisha ongeza sukari na changanya adi kupata ladha uipendayo.

Juisi tayari kwa kunywa,tunza juisi hii frijini ili isiharibike.

011

Unapoandaa juisi hii kwa marayakwanza nashauri uigawanye mara mbili,moja uiwekee tangawizi  na nyingine usiiwekee tangawizi,hii itakupa nafasi nzuri yakuchangua au kuamua ni ladha ipi unapenda zaidi.

HAPPY  NEW YEAR 2014

 

 

JUISI YA UKWAJU


Ukwaju ni tunda ambalo wengi hulitizama kama dawa.Tunda hili linasifika kwa kusaidia kutibu magojwa mbalimbali hii husababishwa na wingi wa virutubisho vinavyopatikana katika tunda hili,hasa madini mwili.

Juisi ya ukwaju

Juisi ya ukwaju

Watu wengi hawapendi juisi ya ukwaju kwasababu ya uchachu mkali na ambavyo inajitenga kwenye glasi (maji huja juu na ukwaju hubaki chini).Unaweza kutengeneza juisi hii na isiwe na uchachu mkali,wala isijitenge kwenye glasi .Juisi huwa nzito na tamu.

Mahitaji

 • Ukwaju robo kilo
 • Parachichi moja –ukubwa wa kati
 • Maji kwa kiasi upendacho
 • Sukari kwa ladha upendayo

Njia

1.loweka ukwaju kwenye maji ,acha uloane kwa saa moja.Tumia mwiko au kijiko kizito kuchanganya na kuponda ukwaju.chuja na weka  pembeni.

 • Ukipenda kutumia mikono,hakikisha umevaa glovzi za jikoni zakushikia vyakula ,si salama kushika na mikono wazi (mara nyingi hutumika mara moja tu kisha unazitupa)
 •   Loweka ukwaju kama uliununua sokoni ukiwa na maganda ukaumenya mwenyewe,kama umenunua ukwaju uliokwisha menywa,badala yakuloweka hakikisha unachemsha ukwaju ukiwa na maji.Lengo ni kuuwa vijidudu vinavyoweza leta magonjwa,kwani unakua umekaa wazi muda mrefu na Hujui aliyeushika kama alikua na mikono safi.

 2.Kata,menya parachichi kisha saga na maji kiasi (tumia mashine yakusagia juisi).chuja  weka pembeni

 • Usiweke parachichi jingi sana,litakata ladha ya ukwaju,weka kiasi tu kwani lengo la kuongeza parachichi ni ili kupunguza uchachu wa ukwaju na kuipa  juice uzito ili maji na ukwaju visitengane.

3.Katika chombo kipana changanya juisi ya ukwaju na parachichi kwa pamoja,ongeza maji adi upate uzito uupendao,ongeza sukari kwa kiasi upendacho kisha changanya adi upate juisi nzuri.isiwe chachu sana,iwe nzito kiasi na hakikisha umeweka sukari yakutosha.Chuja  na Adi hapa juisi tayari kwakunywa.

586

Ukipenda weka frijini iwe baridi.juisi hii inafaa kwa watu warika zote na unaweza kunywa wakati wowote.Kwa wagonjwa wa kisukari au wale ambao wanakwepa kunywa sukari ili kupunguza uzito,unaweza kuweka asali badala ya sukari.

KUNYWA JUISI ILIYOBORA

TIKITI MAJI NA MAZIWA MGANDO (Mtindi)


Kua kwenye diet kunafanya nitafute namna mbalimbali ya kula na kuenjoy vyakula ninavyovipenda.Bila kuharibu juhudi zangu za kupunguza uzito.

katika glasi ni mchanganyiko wa Maziwa mgando,tikiti maji na asali

katika glasi ni mchanganyiko wa Maziwa mgando,tikiti maji na asali

Napenda sana tikiti maji lakini baada ya kula kwa wiki tatu mfululizo ladha yake imeanza kunichosha.leo katika juhudi za kumalizia kipande kilichobaki niliamua kulichanganya kwenye maziwa mgando.

Nimependa sana Ladha yake na nime-enjoy kula.Hii imenipa sababu yakuendelea kula tikiti maji kwa wiki nyingine moja ,uku nikiendelea kuongeza namna mbalimbali za kuenjoy tunda hili.

Mahitaji

 • Maziwa mgando-Nimetumia Tanga fresh
 • Asali
 • Tikiti maji-kata vipande vidogo

Njia

1.weka maziwa kwenye glasi ,ongeza asali kisha korogo ili kuchanganya.

2.chukua glasi nyingine weka vipande vichache vya kitiki maji kisha mimina maziwa kiasi.kisha weka tena matunda na uweke maziwa juu fanya hivyo adi glasi ijae

3.Mwisho kabisa kwa juu,weka vipande vya tikiti maji kisha Nyunyuzia asali.Weka frijini kwa muda kidogo ili iwe baridi.tayari kwa kula.

Maelezo ya ziada

sikuweka vipimo kamili,kua huru kuweka kiasi utakacho.Kwa wale wenzangu tunaopunguza uzito,jali kiasi cha maziwa unayokunywa na kiasi cha asali unachotumia.Nashauri utumie nusu ya paketi ya maziwa (Tanga fresh) na asali kijiko kimoja cha chakula.kama kawaida pima kiasi kwa kuzingatia diet yako.

Unaweza kutumia Nsizi mbivu badala ya tikiti maji au laa ukachanganya matunda yote mawili.

JUISI YA KABICHI NA BEAT ROOTS


Juisi ya mboga za majani si aina ya juisi iniyozoeleka kwa wengi,tumezoea sana kunywa juisi za matunda na baadhi ya mauwa kama rozela.

juisi ya Kabichi na beat roots

juisi ya Kabichi na beat roots

Juisi za mboga ni nzuri sana kwa afya,kwani hubeba virutubisho vingi vinavyoufaa mwili.Naamini unafaham umuhim wa mboga za majani katika afya yako.

Ingawa mboga za majani ni muhim kwa afya ni wazi kwamba watu wengi hawapendi kula mboga za majani,na hawataki hata kujaribu kunywa juisi ya mboga za majani.

Siri kubwa ya kutengeneza juice nzuri ya mboga za majani ni kuhakikisha unaongeza tangawizi,limao au tunda lolote jamii ya limao,apple cider vinegar au apples na Asali.

Tangawizi - hukata harufu kali ya mboga za majani,huipa juice ladha nzuri na huwezesha Metabolism

Limao au matunda jamii ya limao – Hukata harufu ya mboga,huleta uchachu kwenye juice na pia hukupa vitamin C .

Apple cider vinegar – huleta uchachu mzuri sana na pia unapata vitamins na Enzymes wanaoongezwa kwenye vinegar hii,hasa AMERICAN GARDEN apple cider vinegar.Tumia vinegar hii badala ya ya chungwa au limao,na ukipenda waweza weka vyote.

Asali -Tumia Asali badala ya sukari,asali ni sallama zaidi kwa afya kuliko sukari na pia utapata faida nyingi za asali (soma makala ya nyuma juu ya faida za asali)

Juisi hii ni tamu na hata watoto wanaifurahia,ni vizuri ukaongeza ladha ya Vannila ili kukata kabisa harufu ya mboga endapo unaiandaa kwa ajili ya watoto.Hii ni namna nzuri ya kumfanya mtoto apate virutubisho vya mboga za majani

Mahitaji

 • Kabichi ya kijani vikombe 3
 • Kabichi yazambarawe vikombe 3
 • Beatroot 1/2 kikombe.
 • Tangawizi kijiko 1 cha chakula
 • Apple cider vinegar vijiko 3 vya chakula au zaidi (ladha upendayo)
 • Asali kwa ladha upendayo

Njia

1.Osha mboga zote na maji ya moto,kata vipande vidogo kisha weka kwenye mashine ya kusagia juisi.ongeza tangawizi na maji kiasi upendacho kisha saga adi mboga zilainike

2.chuja juisi,kisha ongeza asali na apple cider vinegar,ongeza maji adi upate uzito unaoutaka.changanya vizuri.tayari kwa kunywa.Weka frijini ipate baridi ukipenda.

Tumia mashine ya juisi yaani blender kama hauna mashine ya juisi yaani Juice squeezer.juice squeezer ni nzuri zaidi kwani inakamua juice au maji ya mboga yenyewe hivyo unapata juisi nzuri zaidi.

MBOGA ZA MAJANI NI MUHIM KWA AFYA YAKO

JUISI YA PAPAI


039

Papai ni tunda la kawaida sana katika jamii ya kitanzania.Ni moja kati ya matunda ambayo watu wengi hupanda majumbani .

Papai  linautajiri mkubwa wa Vitamini C,lina vitamin C nyingi kuliko Chungwa.Pia ni tajiri wa vitamini A,vitamin B-complex ,potassium and calcium.Nyama ya tunda hili pia ina nyuzi nyuzi  nyingi (Dietary fiber) ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula mwilini,moja ya sababu zinazofanya papai lisifike kwa kusaidia kutatua tatizo la constipation.

038

Papai huliwa kama tunda,hutumika kutengeneza juisi,hutumika kama kiungo  kwenye vyakula mbalimbali,Hutumika kwenye urembo wa ngozi na pia ni dawa ya  magonjwa mbalimbali ,hasa ya tumbo.

Mahitaji

 • Papai
 • Sukari
 • Maji ya Limao(chugwa au ndimu ukipenda)
 • Maji

Njia

1.Kata papai,toa mbegu zote,toa nyuzi nyuzi nyeupe ambazo hushikilia mbege(Mbegu na nyuzi hizo ni chungu kwa ladha).Menya na katakata .

2.Kamua maji ya limao,weka pembeni

3.katika mashine ya kusagia matunda,weka papai,maji na sukari.Saga pamoja.onngeza maji ya limao ,changanya vizuri .Chuja

 • Weka maji ya limao yakutosha ilii juisi iwe na ladha  ya uchachu.Juisi ikikosa uchachu haiwi nzuri.

037

Juisi tayari kwa kunywa,weka frijini iwe  baridi ukipenda.

JALI AFYA YA FAMILIA YAKO

 

 

 

 

 

KAHAWA BARIDI


014

Ukiishi kwenye miji yenye Joto kama Dar es salaama,ni rahisis sana kupenda kunywa vinywaji vya baridi na kuachana kabisa na vinywaji vyamoto.

Mimi ni mmoja ya watu wasiopenda vinywaji vya moto,Kero kubwa ni lile joto ninalosikia baada ya kunywa kinywaji hicho.Nafurahia  vinywaji vya moto nikiwa kwenye  mikoa yenye baridi kama Arusha,au  kwenye hali ya hewa tulivu kama Mwanza .

013

Hata ivyo ili kuweka mwili wangu  salama,napenda  kunywa maji ya moto au vugu yenye viungo au mitishamba asubuhi ili kuhakikisha Utumbo mwembamba uko salama na unaweza kufanya kazi yake vizuri.

Kila kinywaji kinachonywewa  cha moto,mimi hutafuta namna ya kukifurahia kikiwa baridi.Kama ni  chai ya majani,au chai na maziwa,cocoa,milo,drinking chocolate au kahawa,nitatafuta  tu namna ya kunywa kama kinywaji baridi.

Na hivi ndivyo ninavyokunywa kahawa kama kinwaji baridi:

Mahitaji

 • Maziwa ya Unga vijiko 3 vya chakula
 • Sukari vijiko 2 vya chakula au kwa ladha upendayo
 • Kahawa vijiko 2 vya Chakula
 • Maji glasi 1 na robo
Kahawa iliyoburuzwa ni nzuri kuliko instant coffee(kahawa ya unga laini tunayonunua madukani)

Kahawa iliyoburuzwa ni nzuri kuliko instant coffee(kahawa ya unga laini tunayonunua madukani)

Njia

1.Weka mahitaji yote kwenye sufuria kisha chemsha

2.Maziwa yakileta povu juu,koroga  ili kuzuia yasimwagike .Chemsaha kwa dakika mbili au tatu zaidi ili maji yapungue na kinywaji kiwe kizito.Chemsha kinywaji hiki kwa moto mkali

3.Acha kipoe au pooza.chuja ,weka frijini iwe baridi.Tayari kwa kunywa.

UPISHI NI SANAA, LAZIMA UWE MBUNIFU

 

 

 

 

 

HAPPY MOTHERS DAY:juisi ya mboga za majani


038

Mama,Mother,mom,mammy,maama ni baadhi tu ya namna ya kuita mama.Naamini kila kabila lina namna yake ya kuita mama.kule niilikokulia wanaita Maayo na kule alikotoka mama yangu wanapenda kuita mamaee.Kwa ufupi majina haya hutofautiana kidogo sana.

Kwa kua leo ni siku ya Mama duniani,ni haki na vyema kabisa kusema ASANTE  kwa kina mama wote kwa yote wanayofanya kwaajili ya watoto na familia zao.Katika familia na jamii kwa ujumla mama ananafasi kubwa sana,na tunakila sababu ya kukubali kwamba mama ni nguzo ya familia na ninguzo ya jamii.

Hapa nilipo leo,tabia niliyonayo,utu wangu,uwezo wangu wa kazi,na mengine mengi ni matokeo ya malezi na juhudi za mama.Amekuwepo kwa ajili yangu katika kila hatua ya maisha yangu,nikilia analia na mimi,na nikicheka anacheka na mimi,na kwake Napata upendo usiopimika.Hakuna kubwa sana wala jema sana ninalowezakufanya  ili ajue kwamba nashukuru kwa yote aliyonifanyia na anayonifanyia zaidi ya kusema ASANTE,KUMPENDA NA KUMJALI.

041

Naamini kwamba hata wewe unamengi sana yakusema juu ya mama yako,na unakila sababu ya kumshukuru kwa mengi aliyofanya.Kikubwa Kumbuka Kumwambia Asante kila unapoweza,mpende na ajue kwamba unampenda,mjali na uwepo kwa ajili yake pale anapokuitaji.

Ingawa ni siku ya mama,haitakua haki kama sitawashukuru akina Baba wote pia,kwani Mama hakunilea peke yake,Baba nae ananafasi yake.

Kipekee kabisa,niwape pongezi na hongera kina mama wote wanaojali lishe katika familia zao,wanaochukua muda wao kuingia jikoni na kuandaa chakula kizuri kwaajili ya familia zao.

Asante za kipekee kabisa kwa mama yangu kwa upishi wake bora,na kwakuhakikisha  watoto wake wote wanakua wapishi bora.Kama wewe ni mpenzi wa jiko langu,basi n i vyema ujue kwamba uwezo wangu mzuri wa jikoni nimeutoa kwa mama yangu.Mama ndio mwalim wangu mkubwa wa mapishi na mambo mengine ya jikoni.

022

Sikukuu ya leo kwa kawaida inaambatana na kumpa mama zawadi.Ingawa mama yangu yuko mbali,zawadi niliyomtumia imeshafika.Sijui wewe umempa mama yako zawadi gani?.Kutoka jikoni kwangu kuna zawadi kwa ajili ya akina mama wote.

Kwakua najua moja ya mambo yanayowasumbua kina mama ni namna ya kufanya fwanafamilia wale  mboga za majani basi nawapa zawadi itakayo warahisishia zoezi hilo (wote tunajua watu wengi hawapendi mboga za majani)

Mahitaji

 • Sukuma wiki(tumia sukumawiki change)Majani manne
 • Tango 1/2
 • Tangawizi iliyopondwa kijiko 1 cha chai(tumia tangawizi fresh sio  kavu)
 • Ndimu 3 (au limao)
 • Hoho 1
 • Sukari kwa ladha upendayo
 • Maji.Weka kutokana na uzito wa juisi unaotaka.

015

Njia

1.kamua maji ya ndimu ,weka pembeni.

2.Chemsha maji ya moto sana, tumbukiza sukuma wiki ndani yake , acha kwa dakika moja kisha zitoe.weka pembeni

Nimetumia sukumawiki kutoka bustanini kwangu.Na njia moja ya kuhakikisha mboga ni fesh na hazijawekewa dawa za mimea.

Nimetumia sukumawiki kutoka bustanini kwangu.Na njia moja ya kuhakikisha mboga ni fesh na hazijawekewa dawa za mimea.

3.Kata na changanya,matango,hoho,tangawi,sukuma wiki,maji ya limao,sukari na maji.saga kwa pamoja adi vilainike sana.

 • Usimenye matango.Menya tangawizi.Toa mbegu kwenye hoho.chuja maji ya ndimu.

4.Chuja juisi.Tayari kwa kunywa.

Siri kubwa ya juisi hii ni kuweka limao na tangawizi ya kutosha.Limao huleta uchachu ambao hufanya juisi iwe nzuri,na Tangawizi hukata harufu kali ya mboga za majani mbichi.

Juisi hii ni tamu na imeshehena virutubisho kutoka kwenye mboga za majani.Huna sababu ya kulazimisha wana familia kula mboga,tengeneza juisi ya mboga za majani na utaona kila mtu anaishabikia.Kama hupendi rangi ya kijani kwenye juice,basi unaweza ongeza rangi yoyoye ya chakula.

MUNGU WABARIKI MAMA ZETU

HAPPY MOTHERS DAY.

JUISI YA UBUYU


003

Miaka hii yakaribuni ubuyu umekua tunda lenye jina kubwa sana kwenye jamii yetu ya kitanzania,unasifika kwa kua na virutubisho vingi hasa calcium na Iron

Ubuyu hufaa sana kwa Wajawazito,watoto na wazee,kwani makundi haya yanauhitaji mkubwa wa calcium na iron.

Namna nzuri na rahisi ya kufanya ubuyu sehem ya lishe  ni kwa kuutumia kutengeneza juisi

Juisi ya ubuyu imekua maarufu sana katika jamii yetu na inapendwa sana.Mimi mwenyewe ni mmoja wa wapenzi wakubwa wa juice ya ubuyu.Ingawa unaweza changanya ubuyu na matunda mengine,mimi napenda kunywa juice ya ubuyu pekeyake.Wakati mwingine naiwekea rangi na kuongezea vanila ili tu kuipa sura na harufu ya tofauti.

007

Watu wengi hawachemshi juisi ya ubuyu,Jambo ambalo ni hatarishi ki afya.Chemsha ubuyu ili kuuwa vijidudu viletavyo magonjwa,ubuyu hupita kwenye mikono ya wengi kabla haujakufikia wewe mtumiaji,na pia hujui ulitunzwa katika mazingira gani.Ni vyema kuchukua taadhari kwa kuchemsha.

Mahitaji

Ubuyu(wa unga au wa mbegu)

Maji

Sukari

Njia

1.Chambua ubuyu,ondo uchafu wowote uliopo kwenye ubuyu

2.Katika sufuria,weka ubuyu kisha ongeza maji.Katika kila kipimo cha ubuyu ongeza maji mara tatu yake

 • Ubuyu wa mbegu vikombe 6  weka maji vikombe 9
 • Ubuyu wa unga  vikombe 3 weka maji vikombe 12

3.Funika sufuria kisha bandika jikoni,chemsha adi vitokote,vipe  angalau dakika nne za kutokotea.

002

 • Kumbuka maji unayotumia kuchemsha ubuyu ni maji ya bomba na si salama,hivyo ni muhim kuyapa  muda mzuri wa kuchemka ili juice yako iwe salama.

4.Juisiinapoanza tu kutokota ongeza sukari kwa ladha uipendayo kisha acha zile dakika nne za kutokota ziishe.Zima jiko acha juisi ipoe.

 • Napenda kuweka sukari ichemkie kwenye juice kwani inafanya juice ishikane na kua nzito.Sukari ikichemshwa inakawaida ya kua nzito.Kumbuka kwamba ubuyu ni mwepesi sana na juice yake kawaida hujitenga inapotulia,ubuyu waenda chini na maji yanabaki juu.Ukichemsha sukari inasaidia kuondoa hali hiyo.

5.Chuja juisi,ongeza maji kama unaona ni nzito sana,na ongeza sukari endapo ile uliyoweka awali haitoshi.Juisi tayari kwa kunywa.

006

Maelezo ya ziada.

Kama unampa mtoto mdogo juice hii,basi acha itulie ili unga au chembechembe za ubuyu ziende chini,kisha chukua juisi nyepesi iliyobaki juu nsio umpe mtoto.Juice ya ubuyu nzuri sana kwa mtoto kwani ina calcium kwa wingi.

IFAHAM ROSSELA NA NAMNA YA KUANDAA JUISI YAKE


015

Miaka hii ya karibuni maua ya rosella yamekua na jina kubwa sana hapa nchini.Wengi wamezoea kuyaita maua damu.

Maua ya rosella ni tajiri sana wa vitamin C,A,D,B1,B2,calcium,magnesium,Omega 3,iron,carotene na Assentioal Acids.

Maua haya yanafaida nyingine nyingi,ni dawa na kinga Ya magonjwa mbalimbali kama,kushusha presha,sukari,uric acid na cholestro mwilini,inatibu kikohozi na mafua,inasaidia kupunguza mwili,inatengeneza ngozi na kufanya iwe laini  na mengine mengi.

Maua ya rosella,hutumika kwa mambo mengi,kutengeneza juisi,chai,jam na pipi.Pia hutumika kama rangi ya chakula na hata katika kutengeneza bidhaa za urembo.

Majani ya rosella hutumika kama mboga ya majani na mbegu zake hutoa mafuta yanayoaminika kua dawa nzuri sana ya vidonda.

Ingawa rosella ni kinywaji kizuri sana,watu wengi hukosea kuandaa juisi yake na kusababisha wanywaji wengi wasiipende.Nilichogundua ni kwamba watu wengi huchanganya maji kidogo sana kwenye juisi hii na kuifanya iwe chachu sana,pia wanaweka sukari kidogo sana.

Mara nyingi ninapotembelea nyumba za ndugu jamaa na marafiki,nikipewa juisi ya rosella basi lazima niombe maji na sukari ili nichanganye upya.Lengo si kuwaonyesha kwamba wamekosea bali ni kuwafundisha ili wasikosee tena.

Maua machache sana ya rosella huweza kutoa juisi nyingi sana,Ni aina ya juisi inayofaa sana kwa family.

Juisi kidogo iliyochemswa kwnye sufuria hapo chini(tizama picha zinazofuata).Ilitosha kutengeneza juice sado 3.(ndoo hii kwenye picha)

Juisi kidogo iliyochemswa kwnye sufuria hapo chini(tizama picha zinazofuata).Ilitosha kutengeneza juice sado 3.(ndoo hii kwenye picha)

Maua ya rosella hupatikana madukani,kwenye supermarkets na hata sokoni.Kwa wakazi wa Dar es salaam maua haya hupatikana kwa wingi sana Sokoni kariakoo,kwa kati ya shilling elfu kumi na elfu kumi na mbili kwa kilo.

Mahitaji.

 • Maua ya Rosella
 • Maji
 • Sukari

Njia

1.Katika sufuria weka maua ya rosella pima kwa kutumia kikombe au bakuli,kisha ongeza maji,pima maji mara nne ya kipimo cha maua.Mfano.kama umeweka maua kikombe kimoja basi ongeza maji vikombe vinne.Bandika jikoni,chemsha adi itokote.

007

 • Osha maua kabla ya kuchemsha,sha kwa haraka sana kwani mara tu baada ya kuyaweka kwenye maji yanaanza kutoa rangi,virutubisho na utamu wake.

2.Epua jikoni,acha ipoe.Ikipoa chuja kwa kichujio ili kutenganisha maua na juisi yenyewe

038

 • Ukichuja Akikisha maua yamepoteza rangi nyekundu nakubaki na rangi kama ya pinki,kama maua bado ni mekundu,basi ongeza maji na urudishe jikoni uchemshe tena.
 • 028

3.Ongeza maji kwa kiasi utakacho kwenye juisi hiyo kisha changanya.

032

 • Juisi hii huwa chachu sana,hivyo ni lazima kuongeza maji yakutosha ili kupunguza uchachu huu na kuipa ladha nzuri

4.Ongeza sukari kwa ladha upendayo,kisha changanya vizuri.Na juisi yako itakua tayari.

035

Unaweza kuiweka frijini ili iwe ya baridi,inapendeza sana inapokua baridi.

Maelezo ya ziada-MUHIM KUJUA

1.Namna pekee yakujua kiasi cha maji uliyoongeza kwenye juice yanatosha ni kwa kuonja na kuamua kiasi cha uchachu unaotaka kwenye juisi.Juisi hii ikiwa chachu sana haiwi nzuri.

2.Juisi hii hutumia sukari nyingi,unapoitengeneza weka sukari yakutosha,usibanie sukari.Sukari ikiwa kidogo juisi haiwi nzuri.

3.Nzuri sana Kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano,kwani inavirutubisho vingi,ikiwemo Omega 3 ambayo ni muhim sana kwa mtoto.Hakikisha unampa juisi ikiwa na uchachu kwa mbali.Watoto wa umri huu si wapenzi wa vitu vichachu sana.

4.Kama zilivyo juisi za matunda mengine,juisi ya rosella pia huchacha usipoiweka frijini.

Busara za Tolly

Juisi ya Rosella yenye sukari ikichacha bado inaweza nyweka,kwani kuchacha kwake ni moja ya atua za awali kabisa za kubadili juisi hii kua wine.hivyo kwa wale wanaotumia pombe anaweza kuinywa.Kumbuka kwamba kutengeneza wine kuna kanuni zake pia,ivyo usichachishe  juice makusudu ukimaanisha kutengeneza wine.

Nashauri rosella juice kwa familia ako,kwani licha ya kufuraia utamu wa juice,familia inapata virutubisho vingi kwa mara moja na kwa wakati huohuo mnatibu na kuzuia magojwa.

MAJI NDIO HAYA,KUNYWA NI CHAGUO LAKO.