KARIBU JIKONI

Tollyzkitchen Boresha Mapishi Nyumbani

 

Tolly Ben

Tolly Ben

   UTANGULIZI

Tollyzkitchen ni jiko linalofundisha juu ya chakula na mapishi.Jiko hili huendeshwa na Mtanzania  katika Lugha ya kiswahili kwa ajili ya watumiaji wote wa lugha  ya kiswahili. ……………………………………………………………………..

 

 

MALENGO

Moja:Kuboresha mapishi nyumbani

Ingawa Afrika ni Bara lililobarikiwa na vyakula vingi, Ufahamu na ujuzi wa kuandaa chakula Bora chenye ladha nzuri,muonekano wakuvutia na wingi wa virutubisho ni mdogo kwa waafrika wengi.Jiko hili liko hapa kutatua tatizo hili

Mbili:Kuielimisha jamii juu ya virutubisho vya chakula na umuhimu wake katika mwili.

Elimu ndogo juu virutubisho vya chakula na umuhimu wake katika mwili huwafanya watu wengi wale mlo usio kamili,hivyo kusababisha ukosefu wa virutubisho muhim mwilini na kua chanzo cha magonjwa mbalimbali katika jamii.jiko hili hutoa elimu juu ya virutubisho vya chakula na umuhim wake katika mwili.

Tatu:Kukuza matumizi ya bidhaa za chakula zinazozalishwa Nchini 

Nchi nyingi za Afrika huzalisha bidhaa za chakula. Ingawa bidhaa hizo ni nyingi sana sokoni,watu wengi hupenda kununua na kutumia bidhaa za chakula zitokazo nje.Jiko hili huamasisha waafrika kutumia bidhaa za chakula zinazozalishwa katika nchi zao, kwani bidhaa hizo ni bora na fresh kuliko zile zitokazo nje.Hili litachangia maendeleo na ukuaji wa viwanda vya usindikaji wa  vyakula na kukuza uchumi wa nchi za Afrika

DIRA

Dira ya Tollyzkitchen ni kua jiko linalotoa elimu na mafunzo bora ya upishi,chakula na virutubisho,na kuboresha upishi na ulaji wa virutubisho sahihi vya chakula kwa watanzania na watu watumiao lugha ya Kiswahili.Kuona watanzania wakitumia bidhaa za chakula zinazozalishwa hapa nchini.

DHIMA

 • Kutoa Elimu na mafunzo ya upishi,chakula na lishe bora kwa kupitia,tovuti ,simu,redio ,runinga ,vitabu na mafunzo kwa vitendo.
 • Kutoa ushauri na maelekezo juu ya chakula na lishe kwa makundi maalum
 • Kutoa Elimu juu ya chakula na virutubisho kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ,kwa kushirikiana na taasisi za elimu
 • Kufundisha na kuelimisha jamii juu ya upishi,vyakula na lishe bora kwa kutumia michezo,mashindano,muziki na sanaa mbalimbali.
 • Kukuza na kuboresha matumizi ya bidhaa za chakula zinazozalishwa hapa nchini kwa kutoa elimu ya uelewa na utambuzi wa bidhaa bora za chakula.

KWA MAPISHI NA RECIPES BOFYA  CATEGORIES UIPENDAYO KULIA KWAKO

391 Comments

391 thoughts on “

 1. Elizabeth: majibu ya maswali yako mawili ya mwanzo yako humu kwenye blog, tafadhali soma makala zilizopo.Juu ya mtoto,kuna madarasa kwa njia ya whats app.unaweza kujiunga ili ujifunze juu ya lishe ya mtoto .0769 003 955

 2. Ni leo tu nimeiona hii blog, kwa kweli ninakushukuru kwa kujitoa kutuelimisha. Mungu akubariki sana

 3. huwa napenda sana kufwatilia mapishi ya tollyzkitchen coz yamenisaidia sana na nimegundua kupika vyakula ambavyo nilikuwa sijui! thanks for help us! be blessed

 4. Nataka kujua aina mbalimbali za jinsi ya kupika chakula mtoto kuanzia miez 3-6
  Vyakuka gani wagonjwa wa cansa na presha ya kupanda na kushuka na nk
  Vyakula vya protini ni vpi na wanga ni vpi?
  Ili niwe na afya njema nipike nini au niandalie familiya yangu chakula gni?

 5. napenda kujua mapishi mbali mbali kwa kuanza na jinsi ya kupika crips za viazi mviringo

 6. Judy:Ningejua ambavyo unakanda chapati ingekua rahisi kukusaidia au kukurekebisha.rekebisha haya endapo unafanya vinginevyo, usikande chapati na maji yamoto sana au mafuta yamoto sana, tumia vuguvugu.nitajitaidi kuweka recipe ya chapati soon.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s