Archives

NYAKATI NNE MUHIMU ZA KUNYWA MAJI


maji-yakunywa

Glasi ya maji yakunywa

Kwa kawaida siku haiwezi kwisha pasipo mtu kunywa maji, atakama huta kunywa maji ya kunywa utapata maji kutoka kwenye vinywaji na vyakula utakavyokula kwa siku

Wengi twafaham kua kunywa maji ni muhim kwa ubora na usalama wa afya zetu.Tusilolijua ni kwamba kuna NYAKATI NNE muhim za kunywa maji katika maisha yakila siku, kila unapozembea kunywa maji katika nyakati hizi unahatarisha usalama wa afya yako kwa asilimia kubwa

1.Kunywa glasi mbili za maji  mara tu uamkapo Asubuhi.

Chukua mfano wa injini ya gari, lazima  uweke mafuta yakutosha na uwashe ili ifanye kazi usipofanya hivyo kunauwezekano mkubwa ma uaribifu kutokea . Mwili wako nao hufanya kazi kama injini ya gari, hivyo Kutokunywa maji  asubui ili kuamsha mwili wako nisawa nakuwasha injini bila kuongeza mafuta.

Kunywa glasi 2 za maji  uamkapo asubuhi, amsha mwili wako,uambie kumekucha ni muda wakuanza kazi. Maji huamsha mifumo yote ya mwili na huondoa taka zilizozalishwa mwilini usiku kucha.

Jifunze  kuweka jagi la maji na glasi chumbani kila wakati.

2.Kunywa maji dakika 30 kabla ya kila mlo.

Kunywa maji kabla ya chakula  husaidia katika usagaji wa chakula mwilini, Maji husafisha ulimi na kukuruhusu kufurai ladha ya chakula, huloanisha kuta za mfumo wa usagaji wa chakula na kukuepusha na maumivu ambayo mara nyingi husababishwa na vyakula vyenye asili ya aside, Maji pia hukupa hali yakushiba nakufanya ule chakula kidogo .

3.Kunywa maji  kabla ya kulala usiku

Kunywa maji kabla ya kulala usiku hupunguza uwezekano wakupata mshituko wa moyo /shinikizo la damu.Unapolala usiku mifumo  ya mwili hufanya kazi kama kawaida ,mwili huitaji maji yakutosha ili kuwezesha utendaji wa mifumo hii kumbuka kua asilimia 83 ya mwili wako ni maji, hivyo upungufu wa maji mwilini husababisha mifumo hii isifanye kazi vizuri na kuleta athari.

4.Kunywa maji kila unapohisi mapigo ya moyo yako juu/yameongezeka kwa kasi

Maji yakunywa husaidia kushusha mapigo ya moyo, pale mwili unapopungukiwa maji mapigo ya moyo huenda juu .Mwili hufanya mambo haya mawili pale unapopungukiwa maji. Moja: Mwili hutunza sodiam nyingi  (mwili hufanya sodiam kua mbadala wa maji) hivyo kupandisha mapigo ya moyo. Mbili: Baadhi ya mishipa midodo ya damu ( capillary beds) hufunga nakuacha kufanya kazi pale mwili unapopungukiwa maji na kusababisha msukumo mkubwa wa damu kwenye mishipa mingine ya damu hii hupandisha mapigo ya moyo kwa kasi.

Kunywa maji safi na salama ili kuepuka magojwa .Kumbuka kunywa maji katika nyakati hizi nne ili kuweka afya yako salama zaidi.

imagesNRQCBICM

Ni vyema kufaham kwamba mtu mzima anatakiwa kunywa maji kati ya glasi 8 adi 10 zenye ujazo wa once 8  kwa siku, sawa nakusema vikombe 8 adi 10 kwa siku.

 Once 8 = kikombe 1

Kikombe 1 =glasi 1

JUISI YA LIMAO


juisi-ya-limao

Juisi ya limao

Naamini kila mtu anajua kutengeneza juisi ya limao, nirahisi sana, kamua maji ya limao,ongeza maji na sukari .lakini je.wajua kutengeneza juisi nzuri yalimao yenye ladha na harufu nzuri ya limao ?ijue njia hii ya uakika.

Kanuni ni hii:

kikombe 1 cha sukari kwa kikombe 1 cha maji kwa  kikombe 1 cha  maji ya limao na kijiko 1 cha chakula cha maganda ya limao.

Siri ya kutengeneza juisi nzuri ya limao nikuanza kwa kuandaa syrup ya sukari (maji ya sukari) . Hii husaidia sukari kuyeyuka vizuri  nakufanya juisi iwe naladha nzuri. Limao  lililoiva hutoa juisi nzuri kuliko limao bichi

Malimao mtini

Malimao mtini

Maitaji

 • Sukari kikombe 1 (unaweza punguza kua ¾ ya kikombe)
 • Kikombe 1 cha maji (kwaajili ya syrup)
 • Kikombe 1 maji ya limao
 • Kijiko 1 cha chakula maganda/majani  machanga ya limao
 • Vikombe 3-4 vya maji baridi (yakuchanganyia)

Njia

1.Osha limao, kwakutumia kisu kikali menya maganda ya juu ya limao  bila ganda jeupe la ndani, pima kijiko kimoja cha chakula.

 • Unawezakuumia majani machanga ya limao ,weka majani sita, Osha majani.

2.Katika sufuria dogo changanya maji kikombe kimoja na maganda/majani ya limao kisha funika na bandika jikoni katika moto mdogo.Yakianza kuchemka ongeza sukari kikombe kimoja, koroga adi sukari yote iyeyuke. Zima jiko ,acha ipoe. (hii ndio syrup ya sukari)

 • Ukichemsha kwa moto mkali maganda yalimao yatafanya maji yawe naladha chungu.

3.Wakati syrup inapoa, Kamua malimao  adi upate kikombe kimoja cha maji ya limao.

4.Changanya maji ya limao na syrup ya sukari,kisha chuja ili kutoa maganda na mbegu za limao.Ongeza  vikombe 3 -4 vya maji baridi ,changanya vizuri ,weka frijini kwa dakika 30 adi 40 ili ipoe.

 • Endapo juisi ni tamu sana,ongeza maji ya limao kidogo.Endapo ni kali sana, ongeza maji baridi adi upate ladha upendayo.
 • Ukiongeza maji mengi sana utapoteza ladha na harufu ya limao
 • Kumbuka malimao hutofautiana ladha ya uchachu kutokana na aina ya mbegu ya limao na pale limao hilo lilipolimwa. Hivyo jali kupata  ladha ya uchachu upendayo wewe

5.Weka vipande vya limao na barafu katika jagi unapotenga .

 • Vipande vya limao si kwaajili ya urembo tu,bali pia huongeza  harufu fresh ya limao kwenye juisi wakati wote.

Taarifa

Limao na Ndimu ni matunda mawili tofauti. Watu wengi hudhani Limao na ndimu ni tunda moja.

MAJI YA TANGAWIZI NA MDALASINI


Siku hizi zakaribuni mvua imekua ikinyesha kwa wingi na hali yahewa ni baridi kwa baadhi ya mikoa hapa nchini.Watu hukabiliana na baridi hiyo kwa njia na namna mbalimbali.Hapa jikoni tunakabiliana na baridi kwa kikombe  cha Maji vuguvugu yenye Tangawizi,mdalasini na asali.

015

Tangawizi na mdalasini vinasifa yakuleta joto mwilini kwa haraka na pia huongeza uwezo wa mwili kumeng’enya na kutumia chakula  (Metabolism).Sifa hizi hufanya viungo hivi kua moja ya viungo muhimu katika kuiweka afya yako salama.Unaweza tumia viungo hivi hata katika mapishi mengine

Mahitaji

 • Maji yamoto kikombe 1
 • Tangawizi kijiko 1 cha chai (inaweza kua yaunga,au sugua tangawizi mbichi kisha kamua maji yake)
 • Mdalasini ½ kijiko chai ( wa unga/uliosagwa)
 • Asali Mbichi  kijiko 1 cha chai

Njia

1.Chemsha maji adi yatokote

2.Katika kikombe weka Tangawizi na mdalasini,kisha mimina maji yamoto.Koroga ili kuchanganya.Funika kikombe kwa dakika tano

 •  Funika kikombe ili kutunza virutubisho na kutunza joto ili liwezeshe uvunaji wa virutubisho kwenye viungo
 • Usichemshe viungo jikoni kwani kufanya hivyo kutapoteza virutubisho na nguvu ya viungo

3.Ongeza asali,koroga .Tayari kwa kunywa.

 • Asali huongezwa baada ya joto la maji kupungua ili kuepuka kuuwa enzymes walio kwenye asali,pamoja na kutunza virutubisho vilivyo kwenye asali
 •  Chuja kabla yakunywa ukipenda

Tafiti za Tiba lishe na virutubisho zinaonyesha kwamba ni lazima kutumia tangawizi kijiko kimoja cha chai Wakati wowote unapotumia tangawizi kama tiba lishe ili kupata matokeo

Naamini kinywaji hiki kitakufaa sana siku za baridi

JUISI YA MAEMBE NA UBUYU??!!! HERI YA MWAKA MPYA 2014


HERI YA MWAKA MPYA .Ni mwaka mwingine MUNGU ametupa na tunakila sababu yakumshukuru.Naamini tumeuona mwaka huu kwasababu MUNGU bado anamakusudi na maisha yetu.

Juisi ya Maembe na ubuyu

Juisi ya Maembe na ubuyu

Asante sana kwakua nasi 2013,uwepo wako hapa jikoni umetufikisha hapa tulipo.Kama si kwawapenzi wajiko hili kama wewe basi nina hakika jiko hili lisingekua hivi lilivyo leo. Asante sana kwa sapoti yako na naamini tutakua wote 2014

Ni imani yetu kwamba 2014 utakua mwaka mzuri sana hapa jikoni, Tumejipanga kukupa mambo mazuri na kuboresha upishi wako.

Naamini wengi wetu hufrahia  sana msimu wa maembe unapofika na nihuzuni kwetu msimu huo unapokwisha.Ingawa nijambo la kawaida sana kutengeneza juisi ya matunda mchanganyiko, ni mara chache sana au si kawaida kwa wengi kuchanganya ubuyu na matunda mengine.

Wengi hawahesabu ubuyu katika kundi la matunda  hivyo huwawia vigumu kuwaza kuchanganya ubuyu na matunda mengineili kupata juisi nzuri

Mahitaji

 • Ubuyu (wa unga au mbegu) chemsha na maji  kiasi uku ukikoroga,acha ipoe kisha chuja,weka pembeni
 • Maembe .osha,menya ,kata kisha saga na maji kiasi,chuja,weka pembeni
 • Sukari
 • Maji
 • Tangawizi (kwa anaependa si lazima)

Njia

1.Saga tangawizi iwe laini sana,katika sufuria changanya tangawizi  na maji kiasi,funika sufuria kisha chemsha adi maji yatokote.chuja,acha ipoe.

2..katika chombo kikubwa changanya juisi ya ubuyu na juisi ya maembe na maji ya tangawizi  ,ongeza maji ili kupata uzito uupendao kisha ongeza sukari na changanya adi kupata ladha uipendayo.

Juisi tayari kwa kunywa,tunza juisi hii frijini ili isiharibike.

011

Unapoandaa juisi hii kwa marayakwanza nashauri uigawanye mara mbili,moja uiwekee tangawizi  na nyingine usiiwekee tangawizi,hii itakupa nafasi nzuri yakuchangua au kuamua ni ladha ipi unapenda zaidi.

HAPPY  NEW YEAR 2014

 

 

JUISI YA UKWAJU


Ukwaju ni tunda ambalo wengi hulitizama kama dawa.Tunda hili linasifika kwa kusaidia kutibu magojwa mbalimbali hii husababishwa na wingi wa virutubisho vinavyopatikana katika tunda hili,hasa madini mwili.

Juisi ya ukwaju

Juisi ya ukwaju

Watu wengi hawapendi juisi ya ukwaju kwasababu ya uchachu mkali na ambavyo inajitenga kwenye glasi (maji huja juu na ukwaju hubaki chini).Unaweza kutengeneza juisi hii na isiwe na uchachu mkali,wala isijitenge kwenye glasi .Juisi huwa nzito na tamu.

Mahitaji

 • Ukwaju robo kilo
 • Parachichi moja –ukubwa wa kati
 • Maji kwa kiasi upendacho
 • Sukari kwa ladha upendayo

Njia

1.loweka ukwaju kwenye maji ,acha uloane kwa saa moja.Tumia mwiko au kijiko kizito kuchanganya na kuponda ukwaju.chuja na weka  pembeni.

 • Ukipenda kutumia mikono,hakikisha umevaa glovzi za jikoni zakushikia vyakula ,si salama kushika na mikono wazi (mara nyingi hutumika mara moja tu kisha unazitupa)
 •   Loweka ukwaju kama uliununua sokoni ukiwa na maganda ukaumenya mwenyewe,kama umenunua ukwaju uliokwisha menywa,badala yakuloweka hakikisha unachemsha ukwaju ukiwa na maji.Lengo ni kuuwa vijidudu vinavyoweza leta magonjwa,kwani unakua umekaa wazi muda mrefu na Hujui aliyeushika kama alikua na mikono safi.

 2.Kata,menya parachichi kisha saga na maji kiasi (tumia mashine yakusagia juisi).chuja  weka pembeni

 • Usiweke parachichi jingi sana,litakata ladha ya ukwaju,weka kiasi tu kwani lengo la kuongeza parachichi ni ili kupunguza uchachu wa ukwaju na kuipa  juice uzito ili maji na ukwaju visitengane.

3.Katika chombo kipana changanya juisi ya ukwaju na parachichi kwa pamoja,ongeza maji adi upate uzito uupendao,ongeza sukari kwa kiasi upendacho kisha changanya adi upate juisi nzuri.isiwe chachu sana,iwe nzito kiasi na hakikisha umeweka sukari yakutosha.Chuja  na Adi hapa juisi tayari kwakunywa.

586

Ukipenda weka frijini iwe baridi.juisi hii inafaa kwa watu warika zote na unaweza kunywa wakati wowote.Kwa wagonjwa wa kisukari au wale ambao wanakwepa kunywa sukari ili kupunguza uzito,unaweza kuweka asali badala ya sukari.

KUNYWA JUISI ILIYOBORA

TIKITI MAJI NA MAZIWA MGANDO (Mtindi)


Kua kwenye diet kunafanya nitafute namna mbalimbali ya kula na kuenjoy vyakula ninavyovipenda.Bila kuharibu juhudi zangu za kupunguza uzito.

katika glasi ni mchanganyiko wa Maziwa mgando,tikiti maji na asali

katika glasi ni mchanganyiko wa Maziwa mgando,tikiti maji na asali

Napenda sana tikiti maji lakini baada ya kula kwa wiki tatu mfululizo ladha yake imeanza kunichosha.leo katika juhudi za kumalizia kipande kilichobaki niliamua kulichanganya kwenye maziwa mgando.

Nimependa sana Ladha yake na nime-enjoy kula.Hii imenipa sababu yakuendelea kula tikiti maji kwa wiki nyingine moja ,uku nikiendelea kuongeza namna mbalimbali za kuenjoy tunda hili.

Mahitaji

 • Maziwa mgando-Nimetumia Tanga fresh
 • Asali
 • Tikiti maji-kata vipande vidogo

Njia

1.weka maziwa kwenye glasi ,ongeza asali kisha korogo ili kuchanganya.

2.chukua glasi nyingine weka vipande vichache vya kitiki maji kisha mimina maziwa kiasi.kisha weka tena matunda na uweke maziwa juu fanya hivyo adi glasi ijae

3.Mwisho kabisa kwa juu,weka vipande vya tikiti maji kisha Nyunyuzia asali.Weka frijini kwa muda kidogo ili iwe baridi.tayari kwa kula.

Maelezo ya ziada

sikuweka vipimo kamili,kua huru kuweka kiasi utakacho.Kwa wale wenzangu tunaopunguza uzito,jali kiasi cha maziwa unayokunywa na kiasi cha asali unachotumia.Nashauri utumie nusu ya paketi ya maziwa (Tanga fresh) na asali kijiko kimoja cha chakula.kama kawaida pima kiasi kwa kuzingatia diet yako.

Unaweza kutumia Nsizi mbivu badala ya tikiti maji au laa ukachanganya matunda yote mawili.

JUISI YA KABICHI NA BEAT ROOTS


Juisi ya mboga za majani si aina ya juisi iniyozoeleka kwa wengi,tumezoea sana kunywa juisi za matunda na baadhi ya mauwa kama rozela.

juisi ya Kabichi na beat roots

juisi ya Kabichi na beat roots

Juisi za mboga ni nzuri sana kwa afya,kwani hubeba virutubisho vingi vinavyoufaa mwili.Naamini unafaham umuhim wa mboga za majani katika afya yako.

Ingawa mboga za majani ni muhim kwa afya ni wazi kwamba watu wengi hawapendi kula mboga za majani,na hawataki hata kujaribu kunywa juisi ya mboga za majani.

Siri kubwa ya kutengeneza juice nzuri ya mboga za majani ni kuhakikisha unaongeza tangawizi,limao au tunda lolote jamii ya limao,apple cider vinegar au apples na Asali.

Tangawizi – hukata harufu kali ya mboga za majani,huipa juice ladha nzuri na huwezesha Metabolism

Limao au matunda jamii ya limao – Hukata harufu ya mboga,huleta uchachu kwenye juice na pia hukupa vitamin C .

Apple cider vinegar – huleta uchachu mzuri sana na pia unapata vitamins na Enzymes wanaoongezwa kwenye vinegar hii,hasa AMERICAN GARDEN apple cider vinegar.Tumia vinegar hii badala ya ya chungwa au limao,na ukipenda waweza weka vyote.

Asali -Tumia Asali badala ya sukari,asali ni sallama zaidi kwa afya kuliko sukari na pia utapata faida nyingi za asali (soma makala ya nyuma juu ya faida za asali)

Juisi hii ni tamu na hata watoto wanaifurahia,ni vizuri ukaongeza ladha ya Vannila ili kukata kabisa harufu ya mboga endapo unaiandaa kwa ajili ya watoto.Hii ni namna nzuri ya kumfanya mtoto apate virutubisho vya mboga za majani

Mahitaji

 • Kabichi ya kijani vikombe 3
 • Kabichi yazambarawe vikombe 3
 • Beatroot 1/2 kikombe.
 • Tangawizi kijiko 1 cha chakula
 • Apple cider vinegar vijiko 3 vya chakula au zaidi (ladha upendayo)
 • Asali kwa ladha upendayo

Njia

1.Osha mboga zote na maji ya moto,kata vipande vidogo kisha weka kwenye mashine ya kusagia juisi.ongeza tangawizi na maji kiasi upendacho kisha saga adi mboga zilainike

2.chuja juisi,kisha ongeza asali na apple cider vinegar,ongeza maji adi upate uzito unaoutaka.changanya vizuri.tayari kwa kunywa.Weka frijini ipate baridi ukipenda.

Tumia mashine ya juisi yaani blender kama hauna mashine ya juisi yaani Juice squeezer.juice squeezer ni nzuri zaidi kwani inakamua juice au maji ya mboga yenyewe hivyo unapata juisi nzuri zaidi.

MBOGA ZA MAJANI NI MUHIM KWA AFYA YAKO